ZIARA YA WAFADHILI WA MIRADI
Jopo la Maafisa kutoka Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR), Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), PeaceCorps, DOD na Kituo cha Marekani cha Kudhibiti na Kukinga UKIMWI (CDC) wametembelea Mabinti balehe na akina mama vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24 wilayani Kahama wanaonufaika kupitia mradi wa EPIC unaotekelezwa na Shirika la Family Health International (FHI 360).
Wakiwa wilayani Kahama wakiambatana na viongozi mbalimbali wa Serikali ngazi ya taifa na Mkoa wa Shinyanga maafisa hao wamekutana na vikundi vya mabinti wanaosimamiwa na shirika la Tanzania Development And AIDS Prevention Association (TADEPA) wilayani Kahama pamoja na kujionea shughuli za ujasiriamali zinazofanywa na mabinti hao wakiwemo wasichana 120 wanaosomea masomo ya ushonaji na computer katika kituo salama kwa mabinti.